Blog about the latest automotive news

IGP Afanya Mabadiliko Ya Makamanda Wa Polisi Kwa Baadhi Ya Mikoa

Mkuu wa Jeshi l.  a. Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.

Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ngazi.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Jeshi l.  a. Polisi.

Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi l.  a. Polisi (T)

Makao Makuu ya Polisi.

facebook
[embedded content textile]

twitter
Tweet

google+

linkedin

IGP Afanya Mabadiliko Ya Makamanda Wa Polisi Kwa Baadhi Ya Mikoa

Image source: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixgpma1ml6tkoifc1fZBdQo2b5MCRWGCUN1TofnWE1vWvZ_Jo1MhexaZGx678xyJtiXkFETZT0g-C41SACiyG8fbDg73qsFVR19hwLsNJOI2Jmqo6irg1FO-ZtPuKbGueHvNzIE1mFhOLE/s640/pp.png

Labels: CAR INSURANCE, DONATE CAR

Thanks for reading IGP Afanya Mabadiliko Ya Makamanda Wa Polisi Kwa Baadhi Ya Mikoa . Please share...!

0 Comment for "IGP Afanya Mabadiliko Ya Makamanda Wa Polisi Kwa Baadhi Ya Mikoa "

Back To Top